Thursday, September 25, 2008
Saidi Kibeya akiongelea kuhusu Elimu
Waziri wa Elimu ya taifa na
Utafiti wa Sayansi, Dk Saidi
Kibeya ameongea na HODI
Tanganyika, na kuelezea
mafanikio na matatizo ya
sekta hiyo miaka 3 tangu
ashike wadhifa huo.
Anaanza kwa ufafanuzi wa
sera yq kutoa elimu bila
malipo kwq shule za msingi
iliyoanzishwa rasmi 2005.
Saidi Kibeya: Hatua hii imesaidia
kuongeza idadi ya
watoto wa shule za msingi
kutoka milioni 1 hadi milioni
1 na laki 6 unusu katika miaka
3. Hata hivyo kuna mengi ya
kurekebisha hasa kueneza
mashule sehemu zote za Burundi.
Hatua nyengine ni
kuzidisha uwezo wa serikali
kwa ushirikiano na wafadhili
ambao umesaidia kuongeza
idadi ya masomo kwa mpango
wa kujenga madarasa 2000
kila mwaka, kutafuta waalimu
wenye ujuzi wa kutosha na
kupitia mtala ya usomeshaji,
kuongeza vitabu vya shule.
Kwa sasa, tumefikia kutoa
bila malipo kitabu kimoja kwa
kila watoto 2 wa shule za
msingi kwa matumaini ya kila
mtoto darasani kuwa na kitabu
chake mwenyewe kuanzia
2008-2009.
Tumeanzisha pia masomo ya
Kingereza na Kiswahili na
mafunzo ya kuishi vema
katika jamii, sera ya uzalendo,
haki za binadamu, mazingira
na kupambana na Ukimwi.
Hodi Tanganyika: Ni kipi
unachojivunia zaidi?
S.K: Kubwa kabisa ni kazi ya
ukaguzi na upangaji wa
mfumo mzima wa elimu na
kuweka malengo sahihi ambayo
yatafanya watoto wote
wenye umri wa kwenda shule
wapate haki hiyo kabla ya
2015. Mpango huo unalenga
pia kupambana na umaskini
na ndio daraja Warundi
wanahitaji kulipitia ili elimu
iwe nguzo muhimu ya
maendeleo ya kiuchumi ya
nchi. Ni mpango pia wa raia
wa Burundi kunufaika na
ushirikiano mpya kati ya
Burundi na nchi jirani.
Soma Zaidi Hapa
Courtesy of Hodi Tanganyika News paper
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
I so excited we can also offer swahili news...Thanks JP for hard work
Vugaduhabwe,
Thanks for encouragement,
your blog has inspired a lof of guys on da net.
Hope this kind of item(education) will have a positive impact on Burundian generation
JP
Post a Comment